1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muungano wenye nguvu Tunisia umekosoa mpango wa Rais Saied

5 Januari 2022

Muungano wenye nguvu wa wafanyakazi wa UGTT Tunisia jana umekosoa mpango wa rais Kais Saied, wa kuiondoa nchi hiyo kutoka kwenye mkwamo wa kisiasa, ukisema hauondokani na utawala wa mtu mmoja na utengaji wa wegnine

https://p.dw.com/p/45AHQ
Tunesienn Präsident Kais Saied
Picha: Tunisian Presidency/AA/picture alliance

Rais Kais Saied alisema mwezi uliopita angehimiza kura ya maoni mwezi Julai na kwamba uchaguzi wa wabunge ungefuata mwishoni mwa 2022.

Hayo yanatokea mwaka mmoja baada ya Rais Saied kujipa mamlaka makubwa, hatua ambayo wapinzani wake wanasema ni mapinduzi. Kura ya maoni itafanyika Julai 25, kufuatia mashauriano ya umma mtandaoni ambayo yataanza Januari.

soma zaidi: Tunisia yatumbukia katika mgogoro wa kikatiba

Muungano huo umeendelea kusema kuwa mashauriano ya mtandaoni yaliyopendekezwa na Rais Saied yanaweza kusababisha ukiritimba wa madaraka na kufutwa kwa upinzani.

Tangazo la Saied la jinsi ya kumaliza mgogoro huo limekuwa likisubiriwa tangu aahirishe bunge, kumfuta kazi waziri mkuu na kushika mamlaka tendaji.