Mvutano waongezeka Msumbiji kabla ya idhini ya matokeo
23 Desemba 2024Matangazo
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imekumbwa na machafuko tangu tume ya uchaguzi ilipotangaza kuwa mgombea wa chama tawala cha Frelimo,Daniel Chapo ambacho kimeshika madaraka tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1975 ameshinda katika uchaguzi wa Oktoba 9. Baraza la Katiba linatarajiwa kuyaidhinisha matokeo hayo ya ushindi wa FRELIMO mwendo wa saa tisa alasiri kwa saa za Msumbiji. Daniel Chapo anatarajiwa kuchukua nafasi ya Rais Filipe Nysui ambaye muhula wake wa pili unamalizika Januari 15. Kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane anadai kura ziliibiwa na kwamba yeye na wafuasi wake wataendeleza maandamano ya kupinga matokeo hayo.