1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Mwanafunzi mmoja auawa katika maandamano nchini Senegal

10 Februari 2024

Vikosi vya usalama nchini Senegal vimewafyatulia gesi ya machozi waandamanaji katika mji mkuu Dakar wakati ghadhabu ikiongezeka kufuatia hatua ya kuahirishwa uchaguzi wa urais na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja.

https://p.dw.com/p/4cFTH
Senegal- Maandamano mjini Dakar
Waandamanaji mjini Dakar nchini Senegal wakipinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais: 09.02.2024Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Mwanafunzi huyo aliuawa siku ya Ikumaa katika mji wa kaskazini wa Saint-Louis, hii ikiwa ni kulingana na radio RFM wakati maandamano yakisambaa kote nchini humo.

Polisi walifaýatua gesi ya machozi ili kuwazuia waandamanaji hao waliokuwa wakielekea katikati ya mji wa Dakar, kulikopangwa mkutano waWapinzani wapanga maandamano makubwa Senegal hadhara.

Soma pia: Wapinzani wapanga maandamano makubwa Senegal

Mamia ya waandamaji waliwarushia mawe polisi na kuchoma moto matairi, wakati wakiendelea kuonyesha hasira zao tangu Rais Macky Sall alipotangaza kuahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Februari 25 na ambao sasa utafanyika mwezi Disemba.