1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapinzani wapanga maandamano makubwa Senegal

9 Februari 2024

Wasenegali wamehimizwa leo kujitokeza kwa wingi na kuonesha upinzani wao dhidi ya uamuzi wa kuchelewesha uchaguzi wa rais, katika mtihani wa kupima mizani ya madaraka kati ya Rais Macky Sall na wapinzani.

https://p.dw.com/p/4cEYN
Maandamano ya kupinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi nchini Senegal.
Maandamano ya kupinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi nchini Senegal.Picha: John Wessels/AFP

Dazeni kadhaa za makundi ya kidini na kiraia na mashirika ya kitaaluma, ambayo yameungana katika vuguvugu jipya, yametoa wito kwa watu kuhudhuria swala ya Ijumaa wakiwa wamevalia mavazi meupe na rangi za taifa.

Wakaazi wa mji mkuu wa Dakar, pia wamehimizwa kupitia mitandao ya kijamii, kuandamana baadae leo, kwenye uwanja mkubwa ulioko karibu na mji mkuu.

Soma zaidi: Wabunge wakamatwa wakipinga kuahirishwa uchaguzi Senegal

Utambulisho wa walioitisha maandamano hayo haujabainishwa, lakini wagombea wengi wa uchaguzi ulioahirishwa wametanga kuwa wanapanga kujiunga na maandamano hayo.

Bunge la Senegal liliunga mkono uamuzi wa ghafla wa Sall kusogeza uchaguzi uliokuwa ufanyike tarehe 25 mwezi huu, na kusababisha hasira za wapinzani na wasiwasi wa kimataifa.