1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram kufikishwa mahakamani

28 Agosti 2024

Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram Pavel Durov, amepelekwa mahakamani mjini Paris ambapo anaweza kufunguliwa mashtaka rasmi, baada ya muda wa kwanza wa kukamatwa na kuhojiwa kumalizika.

https://p.dw.com/p/4k1OK
Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram Pavel Durov
Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram Pavel DurovPicha: Tatan Syuflana/AP Photo/picture alliance

Mwanzilishi wa mtandao wa Telegram Pavel Durov, amepelekwa mahakamani mjini Paris ambapo anaweza kufunguliwa mashtaka rasmi, baada ya muda wa kwanza wa kukamatwa na kuhojiwa kumalizika.Telegram yamkamatisha mtuhumiwa ugaidi Ujerumani

Mwanzilishi huyo ambaye ni Mrusi mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Le Bourget, katika mji mkuu wa Ufaransa Jumamosi iliyopita kwa tuhuma za kushindwa kuchukua hatua kudhibiti maudhui hasi kwenye mtandao wake wa kijamii unaotumiwa na watu milioni 900. Kampuni ya Telegram imeyekanusha madai hayo.

Hata hivyo, hatua ya kuwekwa chini ya uchunguzi rasmi nchini Ufaransa hakuna maana ya kutiwa hatiani ingawa uchunguzi huo unaweza kuchukua miaka kadhaa.