Namibia yamchagua rais wa kwanza mwanamke
4 Desemba 2024Matangazo
Tume ya Uchaguzi ya Namibia ECN, imemtangaza Makamu wa Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah, kushinda kwa zaidi ya asilimia 57 ya kura akifuatiwa na mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Patriots for Change IPC, Panduleni Itula aliyepata asilimia 25.5. Itula na chama chake cha IPC lakini wamesema hawatambui matokeo ya uchaguzi huo ambao wanadai ulikumbwa na udanganyifu mkubwa. Nandi-Ndaitwah mwenye miaka 72, anakuwa mwanamke wa kwanza kuitawala nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, iliyoongozwa na chama cha SWAPO tangu ilipopata uhuru mwaka 1990.