1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Nani anadhibiti eneo gani nchini Syria?

5 Desemba 2024

Waasi wenye itikadi kali waliteka maeneo makubwa ya Syria katika mashambulizi ya ghafla yaliyoanzishwa wiki iliyopita. Hatua hiyo imerudisha nyuma mafanikio ya miaka 10 ya vikosi vinavyomtii Rais Bashar al-Assad.

https://p.dw.com/p/4nmaY
Syria | Assad | Hama
Makundi yenye silaha, yanayopinga utawala wa Bashar al-Assad, yanaendelea kusonga mbele na kufanikiwa kuteka maeneo 20 katika jimbo la magharibi la Hama, Syria.Picha: Ibrahim Hatib/Anadolu/picture alliance

Muungano wa wa wanamgambo wenye itikadi kali wa Hayat Tahrir al-Sham (HTS) uliokuwa zamani unaongozwa na tawi la Al-Qaeda la Syria, unatawala ngome ya mwisho ya waasi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Jumatano iliyopita muungano huo na washirika wake, waasi wanaoungwa mkono na Uturuki walianzisha mashambulizi makubwa ya kuuteka mji wa pili wa Syria wa Aleppo pamoja na miji kadhaa na vijiji vilivyokuwa chini ya udhibiti wa serikali.

Mashambulizi hayo yalitokea baada ya miaka ya utulivu tangu serikali iliposhinda katika kampeni za kijeshi zilizoungwa mkono na Urusi.

Waasi wameongeza udhibiti wa maeneo karibu mara mbili kuliko ilivyokuwa awali kabla ya mashambulizi ya hivi karibuni. Hayo ni kulingana na Fabrice Balanche, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Lumiere Lyon kilichopo nchini Ufaransa.

Waasi wachukua udhibiti wa maeneo zaidi

Syria | Khan Assubul | HTS
Wapiganaji wanayoipinga serikali ya Syria wakikamata silaha zilizotelekezwa na jeshi katika mji wa Khan Assubul, Syria, kusini magharibi mwa Aleppo.Picha: Ghaith Alsayed/AP/picture alliance

Mbali na mji wa Aleppo, waasi pia waliingia katikati mwa mkoa wa Hama nchini Syria, huku shirika la kuchunguza vita na haki za binadamu nchini Syria likiripoti mashambulizi mabaya zaidi ya waasi hao katika mji wa Hama.

Mapema katika vita hivyo, serikali ya Bashar Assad ilipoteza udhibiti wa sehemu kubwa ya Syria kwa makundi ya upinzani, wapiganaji wa Kikurdi na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita dola ya kiislamu, IS.

Hatua kwa hatua walianza kurejesha baadhi ya maeneo baada ya kupata msaada wa kijeshi kutoka kwa washiurika wake Iran na kundi la wanamgambo wa Hezbollah kutoka nchini Lebanon.

Soma pia: Vikosi ya serikali vyakabiliana na waasi Hama

Mashambulizi ya hivi punde ya waasi yameufanya mji wa Aleppo kuangukia kwa waasi kwa mara nyingine tena. Jeshi la Syria bado linashikilia eneo la kusini mwa nchi hiyo, likiwemo jimbo la Sweida, ambako maandamano ya kuipinga serikali yametokea mara kwa mara katika mwaka uliopita.

Hata hivyo sehemu ya mkoa wa Aleppo kaskazini bado iko mikononi mwa serikali, pamoja na sehemu za mkoa wa Raqa na karibu nusu ya Deir Ezzor mashariki mwa Syria.

Rais Assad uso kwa uso na viongozi mataifa ya Kiarabu

Vikosi vya serikali vinaungwa mkono najeshi la serikali na wapiganaji wanaoiunga mkono Iran. Iran imesema, inapeleka washauri wa kijeshi nchini Syria kwa mwaliko wa Damascus.

Wanajeshi wa Urusi wamewekwa katika maeneo kadhaa yanayoshikiliwa na serikali, ikiwa ni pamoja na kambi ya jeshi la anga ya Hmeimim karibu na mji wa Latakia kwenye bahari ya Mediterania.

Mnamo mwaka wa 2012, vikosi vya serikali viliondoka katika maeneo yenye Wakurdi wengi kaskazini na mashariki mwa Syria, na kufungua njia kwa Wakurdi kuanzisha utawala wa kujitegemea.

Soma pia: Wanamgambo wa Iraq watua Syria kutoa msaada wa kijeshi

Hatua kwa hatua wamepanua udhibiti wa maeneo yao huku wapiganaji wanaoungwa mkono na Wakurdi wanaoungwa mkono na Marekani wakipambana na kundi linalojiita dola la kiislam la IS, na waliwaondoa wanamgambo hao wenye itikadi kali kutoka kwenye maeneo yao ya mwisho kwenye ardhi ya Syria mnamo 2019.

Tangu mwaka 2016, Uturuki imekuwa ikifanya operesheni za ardhini mfululizo za kuwatimua wanajeshi wa Kikurdi kutoka sehemu za mpaka wa kaskazini mwa Syria. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa muda mrefu amekuwa akitafuta kuanzisha eneo la kilomita 30 ndani ya mpaka wa Syria.