1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO: Urusi iache kuwapeleka wanajeshi mpakani mwa Ukraine

14 Aprili 2021

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameiambia Urusi kuwacha kuwakusanya wanajeshi wake katika mpaka wa taifa hilo na Ukraine huku wanadiplomasia wa juu wa Ukraine na Marekani wakikutana mjini Brussels kwa mazungumzo.

https://p.dw.com/p/3rxEd
Belgien Treffen Dmytro Kuleba und Jens Stoltenberg in Brüssel
Picha: Francisco Seco/AP Photo/picture alliance

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba alisafiri kuelekea Brussels kwa mazungumzo na Jens Stoltenberg siku moja baada ya Ukraine kuishutumu Urusi kupuuza ombi lake la kuwa na mazungumzo kati ya marais wa mataifa hayo mawili, kuhusu kuendelea kuongezeka kwa wanajeshi wa Urusi katika mipaka yake.

Kuleba amesema iwapo Urusi itaendelea kuchukua hatua bila kutafakari au kuanzisha vurugu za aina yoyote ile basi Ukraine itajibu vikali lakini akasisitiza kuwa taifa hilo halitaki vita.

soma zaidi: Urusi yajitetea kujiimarisha kijeshi kwenye mpaka na Ukraine

Akizungumza mjini Brussels baada ya kukutana na Kuleba, Stoltenberg amesema katika wiki za hivi karibuni, Urusi imewapeleka wanajeshi wake katika mipaka hiyo ya Ukraine ambao ni wengi tangu ilipoinyakua rasi ya Crimea mwaka 2014.

Hata hivyo Urusi imesema imefanya hivyo kwa sababu za kujilinda na mara kwa mara imekuwa ikiishutumu Jumuiya ya kujihami NATO kuliyumbisha bara la Ulaya kwa kuwapeleka wanajeshi wake katika mataifa ya Baltic na Poland tangu kunyakulikuwa kwa eneo la Crimea.

Kuleba asema kunahitajika mikakati ya kuuzuwia uchokozi wa Ukraine

Außenminister Maas besucht Ukraine
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Dmytro KulebaPicha: picture-alliance/dpa/V. Ogirenko

Kando na hilo Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema kunahitajika mikakati itakayoizuwia Urusi kuendelea na nia yake ya uchokozi, akipendekeza taifa hilo kuwekewa vikwazo zaidi.

Mkutano wa Kuleba na Stoltenberg ni ishara ya wazi kabisa kwamba Jumuiya ya Magharibi inaiunga mkono Ukraine lakini haikutamka iwapo inaliunga mkono taifa hilo kuwa mwanachama wa NATO.

soma zaidi: Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limeitaka Urusi kuondoa vikosi Crimea

Katibu Mkuu huyo wa NATO pia anatarajiwa kufanya mkutano kwa njia ya video na mawaziri wa mambo ya kigeni na wa ulinzi wa mataifa hayo yanayozozana, hii ikiwa ni kulingana na wanadiplomasia waliohudhuria mkutano wa leo mjini Brussels.

Baadae hii leo maafisa wa Ukraine wanatarajiwa kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken.

Urusi na Ukraine wamekuwa wakilaumiana juu ya mzozo unaoendelea kupanuka Mashariki mwa Donbass ambako wanajeshi wa Kiev wamepambana na wapiganaji wanaoungwa mkono na Moscow katika mgogoro ambao Kiev inasema umesababishwa vifo vya watu 14,000 tangu mwaka 2014.

Chanzo: afp/ap/reuters