Netanyahu akaidi shinikizo la kimataifa
16 Februari 2024Haya yanajiri baada ya ripoti ya gazeti la Washington Post kusema kwamba Marekani, ambayo ni mshirika mkuu wa nchi hiyo, inaendeleza mipango ya kuundwa wa taifa la Palestina.
Katika taarifa iliyochapishwa baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na Rais Joe Biden wa Marekani, Netanyahu amesema kuwa Israel inakataa shinikizo za kimataifa na itaendelea kupinga kutambuliwa kwa upande mmoja kwa taifa la Palestina.
Soma zaidi: Viongozi wa dunia waisihi Israel kuacha operesheni ya Rafah
Hapo jana, Washington Post iliripoti kuwa Marekani inashirikiana na baadhi ya nchi za Kiarabu zikiwemo Misri, Jordan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar na Saudi Arabia, ambayo Israel imetafuta kwa muda mrefu kuanzisha nayo uhusiano wa kidiplomasia, kuhusu mpango wa baada ya mapigano kwa kanda hiyo, ambao utajumuisha ratiba ya kuanzishwa kwa taifa la Palestina.