New York. Rais wa benki ya dunia aomba radhi.
14 Aprili 2007Matangazo
Bodi ya utendaji ya benki kuu ya dunia imesema kuwa rais wake, Paul Wolfowitz , aliamua binafsi wakati akiamuru ongezeko la mshahara lisilokuwa la kawaida kwa mpenzi wake wa kike, ambaye ameajiriwa na benki hiyo.
Pia wamesema watachukua hatua haraka kuamua ni hatua gani wachukue dhidi ya rais huyo wa benki ya dunia.
Wolfowitz ameitisha mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamis na kukiri kuwa alifanya makosa na kuomba radhi kwa kuchukua hatua ya kumpandisha cheo Shaha Riza. Utata huo unatarajia kugubika mkutano wa wiki hii mjini Washington wa benki kuu na shirika la fedha la kimataifa IMF.