Niger yasitisha uchimbaji madini hadi ukaguzi ufanyike
25 Januari 2024Matangazo
Hata hivyo, wizara hiyo haikueleza sababu za kusitishwa kwa utoaji wa leseni katika taarifa yake ya Januari 22 iliyoonekana na shirika la habari la Reuters siku ya Alkhamis (Januri 25).
Waziri wa madhini pia hakutaka kuzungumzia hatua hiyo alipoombwa na shirika hilo.
Taifa hilo la magharibi mwa Afrika lina hifadhi kubwa ya madini ya kiwango cha juu ya urani na ni la saba ulimwenguni kwa kuwa na madini hayo, yanayotumika pia katika utengezaji wa nishati ya nyuklia.
Niger ina kiwanda kikubwa cha usanifishaji urani kinachoendeshwa na kampuni ya Ufaransa ya Orano, ambacho kimeendeleza shughuli zake licha ya mapinduzi ya Julai mwaka uliopita.