Nigeria yajiandaa kwa maandamano kupinga gharama ya maisha
1 Agosti 2024Nigeria inajiandaa kwa maandamano ya nchi nzima ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha, wakati mamlaka zikionya juu ya jaribio lolote la kuiga maandamano ya vijana wa nchini Kenya, yaliyoilazimisha serikali kuachana na muswada wa fedha, ulioazimia kupandisha kodi.
Soma pia: Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya
Maandamano hayo yenye hashtag #EndbadGovernanceinNigeria yamepata uungwaji mkono mkubwa kupitia kampeni ya mitandaoni miongoni mwa raia walioelemewa na gharama za chakula zilizoongezeka kwa asilimia 40 pamoja na bei ya mafuta.
Taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika linakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa sarafu yake ya Naira baada ya Rais Bola Tinubu kuanzisha mageuzi mwaka uliopita yaliyolenga kufufua uchumi uliozorota.