1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yakabiliwa na mripuko wa kutisha wa Kipindupindu

14 Septemba 2021

Nigeria inashuhudia mripuko mbaya zaidi wa maradhi ya kipindupindu ambao haujawahi kuonekana kwa kipindi cha miaka kadhaa.

https://p.dw.com/p/40ILM
Hii ni picha ya maktaba inayoonesha hali ya ukosefu wa maji. Watu wanasubiri kuchota maji katika kisima kimoja eneo la Muna Dalti Maiduguri Nigeria.
Hii ni picha ya maktaba inayoonesha hali ya ukosefu wa maji. Watu wanasubiri kuchota maji katika kisima kimoja eneo la Muna Dalti Maiduguri Nigeria.Picha: picture-alliance/ZumaPress/UNICEF/Gilbertson

Zaidi ya watu 2,300 wamekufa kutoka na maradhi yanayoshukiwa kuwa kipindupindu.

Mripuko huo unashuhudiwa wakati nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikipambana kukabiliana na athari zinazosababishwa na ugonjwa huo pamoja na janga la virusi vya Corona.

Jumla ya visa 69,925 vya ugonjwa wa kipindupindu vimerekodiwa kufikia tarehe 5 ya mwezi huu wa Septemba katika majimbo 25 kati ya majimbo 36 ya nchi hiyo na katika mji mkuu Abuja kwa mujibu wa kituo cha kukabiliana na kudhibiti  magonjwa nchini humo.

Kituo hicho kimeeleza kwamba kiasi watu 2,323 wamekufa kutokana na maradhi hayo kufikia sasa na kuna wasiwasi kwamba idadi kamili huenda ni kubwa zaidi kwasababu jamii nyingi zilizoathirika ziko kwenye maeneo ambayo hayafikiki.

Watoto kati ya umri wa miaka 5 na 14 ndio kundi la walioathirika zaidi katika janga hilo la kiafya.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW