1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria kuanza kutowa chanjo ya Mpox kuanzia Oktoba 8

1 Septemba 2024

Nigeria itaanza kutowa chanjo ya kukabiliana na virusi vya homa ya nyani,Mpox kuanzia Oktoba 8, baada ya udhinishaji wa chanjo hiyo kukamilika nchini humo.

https://p.dw.com/p/4k9C1
Pakistan |Mripuko wa Mpox
Wahudumu wa afya wa Pakistan wakiandaa chumba cha kuwatenga na kuwahudumia walipata maambukizi ya virusi vya Mpox.Picha: Fareed Khan/AP Photo/picture alliance

Nigeria ilipokea dozi shehena ya kwanza ya dozi 10,000 ya chanjo hiyo kutoka shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani siku ya Jumanne wiki hii.

Msemaji wa shirika la maendeleo ya afya ya msingi nchini Nigeria Remi Adeleke amesema chanjo zilizowasili lazima zifanyiwe utafuti wa kimaabara nchini humo kwa kipindi cha wiki tatu na baadae zitaanzakusambazwa katika majimbo matano ambako watu 4,750 watachanjwa,kila mmoja atapata dozi mbili katika muda wa siku 28.

Adeleke amesema wanalenga kutoa chanjo hizo kwa wale walioko kwenye muingiliano wa  karibu na walioambukizwa virusi vya Mpox, wafanyakazi wa afya pamoja na watu wenye kinga dhaifu kiafya.