1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu fainali ya EURO 2024 itakuwa patashika

7 Julai 2024

Timu ya soka ya Uholanzi imejikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya kandanda kwa maitaifa ya Ulaya EURO 2024 baada ya kuibamiza Uturuki mabao 2-1.

https://p.dw.com/p/4hymn
Euro 2024 | Uturuki na Uholanzi
Uholanzi imejikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya kandanda kwa maitaifa ya Ulaya EURO 2024 Picha: Odd Andersen/AFP/Getty Images

Ushindi huo katika mchezo uliopigwa mjini Berlin umefufua matumaini ya timu hiyo kulikaribia kombe la EURO ambalo walilinyakua kwa mara ya mwisho mwaka 1988. 

Uholanzi itakuwa na kibarua kigumu pale itakapokutana na England kwenye mchezo wa nusu fainali uliopangwa siku ya Jumatano ya wiki ijayo. 

Euro2024: Uhispania yawatoa wenyeji Ujerumani robo fainali

England nayo ilisonga mbele hapo jana kupitia mikwaju ya penalti ya 5-3 katika mchezo uliowakutanisha na timu ya taifa ya Uswisi. Timu nyingine mbili zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni Ufaransa na Uhispania ambazo zina miadi mnamo siku ya Jumanne. 

Ufaransa ilipata ushindi dhidi ya Ureno kupitia penalti na Uhispania iliwafungasha virago wenyeji Ujerumani kwa mabao 2-1.