Pakistan, Saudi Arabia zasaini mikataba ya mabilioni ya dola
11 Oktoba 2024Mikataba hiyo inahusisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, teknolojia, kilimo, madini, afya na nishati.
Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, na mkuu wa majeshi mwenye ushawishi mkubwa, Jeneralli Asim Munir, walishuhudia sherehe za utiaji saini zilizofanyika jana mjini Islamabad.
Soma zaidi: Wafuasi wa Imran Khan wakabiliana na polisi Islamabad
Sharif alisema kwenye hotuba yake kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha mikataba hiyo inatakelezwa kikamilifu. Sharif aliishukuru Saudi Arabia kwa kuisaidia kupata mkopo wa dola bilioni saba kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Makubaliano hayo yamesainiwa siku moja tu baada ya Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia, Khalid al-Falih, kuwasili nchini Pakistan.
Islamabad imekuwa na uhusiano mzuri na Riyadh, ambayo inaongoza kwa uuzaji mafuta nchini Pakistan.