Poland na Hungary zaukosoa uamuazi wa mahakama ya Ulaya
16 Februari 2022Matangazo
Waziri wa Sheria wa Hungary Judit Varga kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter ameutaja uamuzi huo kama "uliochochewa kisiasa" na "ushahidi hai kwamba Umoja wa Ulaya unatumia vibaya madaraka yake."
Hungary inasema inaadhibiwa kutokana na sheria tata kuhusu wapenzi wa jinsia moja iliyoipitisha mwaka jana.
Naye Waziri wa Sheria wa Poland Zbigniew Ziobro amesema Umoja wa Ulaya unaelekea kuwa chombo ambacho nguvu inaweza kutumika kuwanyima na kubana uhuru wa nchi wanachama.
Uamuzi huo uliotolewa na mahakama hiyo iliyoko Luxembourg unamuwekea shinikizo Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen kufanya uamuzi wa iwapo na ni lini ataanza kuutekeleza.