1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland yaimarisha ulinzi katika eneo la mpakani na Belarus

3 Julai 2023

Poland imepeleka maafisa zaidi wa polisi kwenye mpaka wake na Belarus. Waziri wa mambo ya ndani Mariusz Kaminski amesema hatua hiyo ni muhimu ili kuimarisha usalama kutokana na kile alichokiita hali ya wasiwasi.

https://p.dw.com/p/4TLIA
Polen | Grenze zu Belarus
Picha: Wojtek Radwanski/AFP/Getty Images

Kupelekwa mpakani kwa polisi wa ziada 500 kunajiri baada ya naibu Waziri Mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski kusema anaamini kuwa tayari kuna wanajeshi 8,000 wa kampuni ya mamluki ya Kirusi ya Wagner nchini Belarus.

Kaczynski amesema polisi hao wa ziada wataongeza kwa idadi ya walinzi 5,000 wa mpakani na wanajeshi 2,000. Rais wa Belarus Alexander Lukashenko alisema wiki iliyopita kuwa kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin aliwasili nchini mwake.

Soma pia:MSF yaondoka mpaka wa Beralus na Poland 

Hatua hiyo ilizusha wasiwasi miongoni mwa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO yanayopakana na Belarus, ambayo ni Poland, Latvia na Lithuania.