1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto mkubwa wazuka kwenye maghala mawili mjini Hamburg.

9 Aprili 2023

Polisi na idara ya zima moto katika mji wa bandari wa Hamburg nchini Ujerumani zimetoa tahadhari kwa wakaazi wa mji huo juu ya uwezekano wa kusambaa sumu hewani baada ya moto mkubwa kuzuka katika maghala mawili.

https://p.dw.com/p/4PrAx
Großbrand in Hamburg
Picha: Lutz Faupel/REUTERS

Polisi na idara ya zima moto katika mji wa bandari wa Hamburg nchini Ujerumani zimetoa tahadhari leo Jumapili kwa wakaazi wa mji huo juu ya uwezekano wa kusambaa sumu hewani baada ya moto mkubwa kuzuka katika maghala mawili kwenye wilaya ya Rothenburgort mashariki mwa Ujerumani. Maghala hayo mawili kwenye eneo la kuegesha malori yalianza kuteketea moto tangu saa kumi alfajiri, kulingana na msemaji wa polisi. Wakati huo huo, polisi wamesema watu 140 wamehamishwa kutoka wilaya hiyo ya Rothenburgsort, iliyo kilometa chache kutoka katikati ya  jiji la Hamburg. Shirika la reli la Ujerumani, Deutsche Bahn, limesema limefunga njia kati ya Hamburg na mji wa karibu wa Büchen kutokana na moto huo na pia treni kati ya Hamburg na Berlin pia zimebadilishwa njia na hivyo zinaweza kuchelewa kufika kwa wakati kwa muda wa hadi saa nzima.