1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Kenya yawatawanya waandamanaji wanaopinga utekaji

30 Desemba 2024

Polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi imewafurumusha kwa mabomu ya machozi na kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana leo Jumatatu dhidi ya kile wanachosema kuongezeka kwa wimbi la utekaji nyara

https://p.dw.com/p/4ogwt
Kenia Kenianische Aktivisten demonstrieren in Nairobi gegen ein unpopuläres Finanzgesetz
Wanaharakati wakijibu baada ya maafisa wa polisi wa kutuliza ghasia kuvamia vitoa machozi ili kuwatawanya,katikati mwa jiji la Nairobi, Kenya Juni 6, 2023.Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi imewafurumusha kwa mabomu ya machozi na kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakiandamana leo Jumatatu dhidi ya kile wanachosema kuongezeka kwa wimbi la utekaji nyara dhidi ya wakosoaji wa serikali ya William Ruto, Shirika la habari la Reuters limesema. Kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binadamu ni kwamba makumi ya Wakenya wametekwa nyara katika miezi ya hivi karibuni, wengi wao wakiwa wanawalaumu polisi na idara za ujasusi kwa kuhusika na matukio hayo. Mamlaka za Kenya zimejitokeza na kujibu shutuma hizo zikidai kuwa serikali haiungi mkono na wala haihusiki kwa namna yeyote juu mauaji ya kiholela pamoja na utekaji nyara. Baadhi ya makundi ya vijana waandamanaji waliandamana katikati mwa jiji la Nairobi huku wengine wakiwa wameweka kambi na kuimba nyimbo za kuipinga na kuikashifu serikali,matukio hayo ni kulingana na picha zilizoonyeshwa kwenye shirika la utangazaji la NTV la nchini humo.