1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Ujerumani yafanya msako wa wasafirishaji wahamiaji

5 Desemba 2024

Polisi nchini Ujerumani imefanya msako dhidi ya mtandao wa kihalifu wa Wakurdi wenye asili ya Iraq unaotuhumiwa kusafirisha wahamiaji kwa boti kutoka Ufaransa kwenda Uingereza.

https://p.dw.com/p/4nlJ9
msako, Ujerumani
Operesheni ya msako ya polisi ya Ujerumani.Picha: IMAGO/Revierfoto

Zaidi ya maafisa 500 waliendesha msako kwenye miji kadhaa ya magharibi mwa Ujerumani wakishirikiana na maafisa wa polisi ya Ulaya, Europol, na wa Ufaransa.

Mtandao huo wa wahalifu unashutumiwa kuwasafirisha wahamiaji haramu kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Mashariki kuelekea Ufaransa na Uingereza wakitumia mashua mbovu, kwa mujibu wa taarifa ya polisi ya Ujerumani.

Soma zaidi: Boti tisa za wahamiaji zakamatwa zikijaribu kuingia Uingereza

Miongoni mwa miji iliyokumbwa na msako huo ni Essen, Gelsenkirchen, Grevenbroich na Bochum.

Gazeti mashuhuri la Bild la Ujerumani limeripoti kwamba msako huo wa jana Jumatano ulihusu pia kambi moja ya wakimbizi mjini Essen.