1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Chad kushiriki uchaguzi katika mazingira magumu

24 Desemba 2024

Raia wa Chad wanajitayarisha kushiriki uchaguzi wa rais na bunge Jumapili ya tarehe 29 Desemba. Serikali ya rais Mahamat Idriss Deby Itno imesema uchaguzi huo ni sehemu ya hatua muhimu ya mabadiliko ya kidemokrasia.

https://p.dw.com/p/4oYQz
Mahamat Deby Itno
Raia wa Chad kushiriki uchaguzi katika mazingira magumu Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Uchaguzi huo unafanyika huku kukiwa na visa vya mara kwa mara vya mashambulizi ya makundi ya jihadi ya Boko Haram katika eneo la ziwa Chad, kumalizika kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya taifa hilo na koloni lake la zamani Ufaransa na shutuma za kujiingizaa katika mgogoro wa taifa jirani la Sudan. 

Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa kunawatia wasiwasi Wachad

Upinzani unaosusia uchaguzi huo umeituhumu serikali kuwa ya kiimla na kandamizi. Upinzani kupitia kiongozi wa chama cha Transformers, Succes Masra amesema kushiriki uchaguzi huo chini ya hali ilivyo sasa  ni kama kushiriki uchaguzi usio wa haki.

Uchaguzi unafanyika wakati waandishi habari wakiandamana na kugoma kupinga kunyimwa uhuru wao.