SiasaVisiwa vya Comoros
Raia wapiga kura kwenye visiwa vya Comoro
14 Januari 2024Matangazo
Watu wapatao laki tatu na arobaini elfu wamejiandikisha kupiga kura kwenye visiwa hivyo vyenye wakaazi laki nane.
Wapinzani wanadai kwamba tume ya uchaguzi inakipendelea chama tawala, madai ambayo tume hiyo imeyakanusha na imeeleza kuwa uchaguzi utafanyika kwa njia ya uwazi.
Rais Assoumani ambae hapo awali alikuwa afisa wa jeshi alitwaa madaraka mnamo mwaka 1999. Na tangu mwaka huo ameshinda katika chaguzi tatu.
Alishinda kwa kupata asilimia 60 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2019.