1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Rais Assoumani wa visiwa vya Comoro ashinda muhula wa nne

17 Januari 2024

Rais wa visiwa vya Comoro Azali Assoumani ameshinda muhula wa nne madarakani baada ya tume ya uchaguzi kutangaza matokeo ya mwisho ya kura iliyofanyika mnamo Jumapili iliyopita.

https://p.dw.com/p/4bLTc
Visiwa vya Comoro | Azali Assoumani
Rais Assoumani wa visiwa vya ComoroPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Matokeo yaliyotangazwa jana jioni yanaonesha Assoumani ameshinda kwa asilimia 62.7 ya kura. Upinzani mara moja umeyapinga matokeo hayo ukilalamika kwamba uchaguzi wote uligubikwa na dosari ikiwemo vituo kufungwa kabla ya muda uliowekwa kisheria.

Mmoja ya wanagombea watano wa upinzani Mouigni Baraka Soilihi, amesema hawawezi kuyakubali matokeo yaliyotangazwa kwa sababu ya hitilafu zilizoshuhudiwa ikiwemo tuhuma za wizi wa kura. Tume ya uchaguzi imeyapinga madai hayo ya upinzani.

Rais Assoumani amekuwa madarakani tangu mwaka 2016 na alirefusha muhula wake kupitia mabadiliko tata ya katiba ya mwaka 2019, yaliyoondoa sharti la nafasi ya urais kuwa ya kupokezana miongoni mwa visiwa vitatu vikubwa vinavyounda Jamhuri ya Comoro.