Rais Macron kufanya ziara rasmi Ujerumani Mei 26
2 Mei 2024Matangazo
Safari ya Macron ilifutwa kutokana na maandamano makubwa yaliyoshuhudiwa nchini Ufaransa kufuatia mauaji ya kijana Nahel.
Macron na mkewe Brigitte wanatarajiwa kuwasili Berlin Mei 26 na watapokelewa kwa heshima zote za kiitifaki katika Ikulu ya Bellevue na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mkewe Elke Büdenbender.
Soma pia:Macron: Ulinzi wa Ulaya unapaswa kuwa zaidi ya NATO
Hii itakuwa ziara ya kwanza ya kiserikali kufanywa na rais wa Ufaransa tangu ile iliyofanywa na hayati Jacques Chirac mnamo mwaka 2000.
Mjini Berlin, Macron atahudhuria tamasha litakalofanyika kwenye Bunge la Ujerumani Bundestag kuashiria maadhimisho ya miaka 75 ya katiba ya nchi hii.