Rais mpya wa Senegal aapishwa rasmi
2 Aprili 2024Sherehe za kuapishwa kwake zimefanyika katika mji mpya wa Diamniadio, karibu na mji mkuu Dakar.
Faye mwenye umri wa miaka 44, ambaye anakuwa rais kijana zaidi kuwahi kuliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi, amekula kiapo mbele maafisa wa Senegal pamoja na wakuu wa nchi kadhaa za Kiafrika.
Soma zaidi: Faye analenga kuibadilisha Senegal kiuchumi kwa kutumia gesi na mafuta
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi, Faye ambaye ni mshirika mkuu wa kiongozi maarufu wa upinzani, Ousmane Sonko, alisema vipaumbele vyake ni maridhiano ya kitaifa, kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha na kupambana na ufisadi.
Lakini changamoto kubwa inayomkabili itakua kukabiliana na viwango vya ukosefu wa ajira, hasa kwa vijana ambao ni karibu asilimia 75 katika nchi yenye watu milioni 18.