Rais Putin atazamiwa kufanya ziara nchini China mwezi Mei
19 Machi 2024Rais wa Urusi Vladimir Putin anatazamiwa mwezi Mei kuelekea chini China na kukutana kwa mazungumzo na Rais Xi Jinping, katika ziara ambayo inaweza kuwa ya kwanza ya kiongozi huyo wa Kremlin nje ya nchi katika muhula wake mpya wa urais.
Serikali za Magharibi zimekosoa hapo jana kuchaguliwa tena kwa Putin na kusema mchakato wa uchaguzi haukuwa huru, wala wa kidemokrasia. Lakini China, India na Korea Kaskazini zilimpongeza kiongozi huyo ambaye pia ni mshirika wao, kwa kuendeleza utawala wake kwa miaka sita zaidi.
Sherehe rasmi za kuapishwa Putin zinatarajiwa kufanyika Mei 7 mwaka huu. Katika miaka ya hivi karibuni, China imeimarisha uhusiano wake wa kibiashara na kijeshi na Urusi, huku Marekani na washirika wake wakiziwekea vikwazo nchi hizo mbili, haswa Moscow, kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.