Rais Steinmeier asifu mageuzi ya kiuchumi ya Nigeria
12 Desemba 2024Matangazo
Katika siku ya kwanza ya ziara ya Steinmeier katika nchi tatu za Afrika, Tinubu amesisitiza kuwa Nigeria imeanzisha mageuzi yanayounufaisha uchumi katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kupunguza urasimu na mageuzi ya kodi.
Akiwa mjini Abuja, Steinmeier amepongeza juhudi za Nigeria, akisema mageuzi hayo yanachukuliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa Ujerumani kama kuimarishwa kwa uhusiano wa uwekezaji.
Steinmeier amesema Nigeria yenye watu takribani milioni 220, ni mshirika wa pili kwa ukubwa wa kibiashara wa Ujerumani katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kabla ya kukutana na Tinubu, kiongozi huyo wa Ujerumani alikutana na Omar Touray, Rais wa Jumuia ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.