Rais Putin akutana na naibu waziri mkuu wa Serbia
4 Septemba 2024Matangazo
Mkutano wa viongozi hao unafanyika wiki moja baada ya serikali ya mjini Belgrade kusaini mkataba wa mabilioni ya dola wa ndege za kivita na Ufaransa.
Naibu waziri mkuu wa Serbia Aleksander Vulin amesema nchi yake haiwezi kuwa mwanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO, lakini pia haitothubutu kuiwekea vikwazo Urusi na pia haitoiruhusu kutumiwa katika hatua zozote dhidi ya Urusi.
Soma pia:Serbia yamuahidi Putin kwamba kamwe haitaigeuzia mgongo
Urusi na Serbia zina mahusiano ya karibu kihistoria. Nchi hiyo pia imeendelea kujitenga na Umoja wa Ulaya katika hatua za kuiwekea vikwazo Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine.