Rais wa Iran kumtembelea Mfalme wa Saudi Arabia
20 Machi 2023Matangazo
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Hossein Amirabdollahian amesema kuwa Tehran imependekeza sehemu tatu za kufanyika mkutano na mwenzake wa Saudia.
Iran na Saudi Arabia zilikubaliana kurejesha mahusiano na kuzinfungua balozi zao mnamo Machi 10 mwaka jana katika muafaka uliosimamiwa na China.
Soma pia: Nchi kadhaa zasifu hatua ya Iran na Saudia kufufua uhusiano
Nchi hizo mbili kwa miaka mingi zimekuwa zikigombea ushawishi katika Mashariki ya Kati, kwa kuunga mkono makundi pinzani katika vita vya nchini Yemen na Syria.
Wakati huo huo, Iraq na Iran zimesaini makubaliano ya kuimarisha usalama wa mpakani. Makubaliano hayo yalitangazwa jana na ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.