Rais wa Poland aikosoa Ulaya kwa kufungia fedha zake
21 Januari 2024Matangazo
Serikali ya zamani ya Poland iliyoongozwa na chama cha kizalendo cha sheria na haki (PiS) ilihusika katika mvutano na Umoja wa Ulaya juu ya mageuzi ya mahakama na mfumo wa sheria hali iliyosababisha mabilioni ya fedha za Poland kuzuiliwa na Umoja huo.
Donald Tusk aapishwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Poland
Serikali mpya inayounga mkono Umoja wa Ulaya, imeahidi kupata nafasi ya kufikia tena fedha hizo kwa kurejesha utawala wa sheria lakini inakabiliwa na changamoto kutoka kwa wafuasi na washirika wa chama cha serikali ya akiwemo Duda na majaji wengine mashuhuri.
Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya haikupatikana kutoa maoni juu ya taarifa hii.