Rais wa Senegal afanya ziara ya kwanza nchini Nigeria
17 Mei 2024Nigeria na Senegal zimesisitiza kukuza demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi wakati Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye Faye alipofanya ziara yake ya kwanza rasmi. Haya ni kulingana na ofisi ya Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu.
Eneo la Afrika Magharibi limeshuhudia mapinduzi kadhaa ya kijeshi na kwa mujibu wa taarifa rasmi ya ofisi hiyo ya rais. Kiongozi wa Nigeria Tinubu, amesema kuwa nchi yake na Senegal zilikuwa na nia moja kuhusu demokrasia na kwamba Senegal imeudhihirishia ulimwengu kuhusu demokrasia ya kikatiba.
Ziara alizozifanya tangu achaguliwe: Bassirou ziarani Mauritania, Gambia
Kulingana na taarifa hiyo, Rais Faye pia alisisitiza kujitolea kuyashaiwshi mataifa yaliokumbwa na mapinduzi ya kijeshi kurudi na kushiriki maadili yao ya kawaida ya kidemokrasia na kile wanachokisimamia.
Ofisi hiyo ya Rais wa Nigeria, imesema Rais Faye ameongeza kwamba Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, ambayo Tinubu ni mwenyekiti wake, inapitia wakati mgumu lakini bado kuna matumaini.