1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia kushinda muhula wa pili madarakani

7 Oktoba 2024

Rais wa Tunisia Kais Saied amesema atasubiri matokeo rasmi ya uchaguzi, kabla ya kujitangaza mshindi, huku akiyatambua matokeo ya awali ya kura yanayonesha ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa urais.

https://p.dw.com/p/4lUUR
Rais wa Tunisia Kais Saied
Rais wa Tunisia Kais Saied Picha: Fauque Nicolas/Images de Tunisie/ABACA/picture alliance

Wafuasi wa Kais Saied tayari wameanza kusherehekea kwa kupiga honi barabarani muda mfupi tu baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika huku televisheni ya kitaifa ikioyesha vidio  za rais Saied akiahidi kukabiliana na wasaliti na wale wanaopanga matukio mabaya dhidi ya Tunisia, akionekana kuendelekza kile alichokuwa anakjifanya katika uongozi wake.  Saied alionekana akisema ataisafisha nchi kwa kuwaondoa watu wote waliowafisadi na wapangaji njama dhidi ya taifa hilo. 

Kulingana na kura ya maoni iliyotangazwa na televisheni ya taifa nchini humo  kutoka kwa shirika la kibinafasi la Sigma Conseil, ambalo limekuwa likichapisha matokeo ambayo hayapishani sana na matokeo rasmi, Ilimuonyesha rais huyo wa Tunisia akishinda kwa zaidi ya asilimia 89 ya kura akiwashinda wapinzani wake waliofungwa jela mwanabiashara Ayachi Zammel na Zouhair Maghzaoui kutoka chama cha mrengo wa kushoto aliemuunga mkono Saied kabla ya kuamua kupambana nae katika uchaguzi huu wa rais. Tume ya uchaguzi nchini humo iliwapiga marufuku wagombea 14 wa urais kuingia katika kinyanganyiro hicho ikisema hawakuidhinishwa kwa wingi.

Katika taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika linalojulikana kama chimbuko la vuguvugu la kiarabu, wengi wa wapinzani waliamua kuususia uchaguzi huo wakiuita wa kini macho kufuatia wakosoaji wa rais huyo kufungwa jela pamoja na waandishi habari, mawakili, wanaharakati na viongozi kadhaa wakuu wa mashirika makubwa ya kiraia nchini humo. Hali hiyo imesababisha idadi ya waliojitokeza kushiriki uchaguzi kuwa ndogo.

Idadi ndogo ya watu yashiriki uchaguzi

Tunesien | Uchaguzi wa rais
Upinzani wasusia uchaguzi baada ya wagombea wao kufungwa jelaPicha: Zoubeir Souissi/REUTERS

Wakati vituo vya kupigia kura vilipofungwa watu milioni 2.7 ambao ni sawa na asilimia 27.7 ndio waliokuwa tayari wameshapiga kura zao ambayo ni idadi ndogo ikilinganishwa na asilimia 49 ya waliojitokeza kupiga kura katika awamu ya kwanza ya uchaguzi uliopita wa urais wa mwaka 2019. Farouk Bouasker mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tunisia anathibitisha hilo.

" Idadi jumla ya waliojitokeza kupiga kura  ilipofika saa 12 jioni  ilikuwa ni ya watu 2,704,155, ya wanawake na wanaume wa Tunisia  walipiga kura ndani na nje ya nchi kama inavyoonekana katika kiruninga kidogo"

Matakeo rasmi yanatarajiwa kutolewa Jumatatu (07.10.2023) 

Miaka mitatu baada ya rais Saied kujilimbikizia madaraka, watetezi wa haki za binaadamu wanahofia kuwa kuchaguliwa kwake tena kuendelea kuiongoza nchi hiyo utaendeleza uongozi wake wa kiimla katika nchi ambayo ilikuwa ya kwanza kumuondoa rais dikteta wa muda mrefu Zine El Abidine Ben Ali kupitia maandamano makubwa dhidi ya utawala wake mwaka 2011. Wanaharakati wanasema hali inaendelea kuwa mbaya nchini humo iliyoanza baada ya kuchaguliwa kwa Kais mwaka 2019. 

Afp/ap