1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Rais wa UAE kwa Assad: Ni wakati wa Syria kurejea Uarabuni

20 Machi 2023

Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan amemwambia mwenzake wa Syria Bashar al-Assad kuwa wakati umefika kwa nchi yake ambayo imetengwa kidiplomasia kurejeshwa katika ulimwengu wa Kiarabu.

https://p.dw.com/p/4OvIl
Vereinigte Arabische Emirate | Syriens Präsident al-Assad zu Besuch in Abu Dhabi
Picha: Syrian Presidency/apaimages/IMAGO

Ziara ya al-Assad mjini Abu Dhabi ni ya pili katika Umoja wa Falme za Kiarabu katika miaka mingi na imejiri baada ya kuzuru Omar mwezi uliopita, zikiwa ndio ziara zake pekee rasmi katika nchi za Uarabuni tangu kuanza kwa vita vya Syria mwaka wa 2011.

Nahyan amemwambia Assad kuwa Syria imekuwa mbali na ndugu zake kwa muda mrefu, na wakati umewadia wa kurejea kwao na katika mazingira yake ya Kiarabu.

Soma pia: Rais wa Syria Bashar al-Assad awasili Abu Dhabi katika ziara rasmi ya kiserikali.

Rais huyo wa Falme za Kiarabu ametoa wito wa juhudi za kuwezesha kurejeshwa makwao wakimbizi wa Syria na akaidhinisha ushirikiano wa Damascus na Ankara, ambayo sasa inafanya kazi kuelekea maelewano na Assad baada ya miaka mingi ya kuwaunga mkono waasi wanaopigana na serikali yake.