1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asema majeshi yake yamesonga mbele huko Kursk

14 Agosti 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema majeshi ya nchi yake yanasonga mbele kwenye jimbo la Urusi la Kursk, baada ya kuanzisha mashambulio ya kushtukiza wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4jSvS
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Sergei Supinsky/AFP/Getty Images

Zelensky ameeleza kuwa wanajeshi wa nchi yake wanasonga mbele kilometa moja hadi mbili katika kila upande tangu kuanza kwa mashambulio.

Amesema askari wa Urusi zaidi ya100 wametekwa. Rais huyo wa Ukraineameongeza kusema kwamba hatua hizo zitaharakisha kurejea nyumbani kwa wanajeshi wake.

Wakati huo huo Urusi imesema imeyarudisha nyuma majeshi ya Ukraine yaliyojaribu kupenya ndani zaidi katika maeneo matano ya jimbo la Kursk.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vya Ukraine vya mwendo kasi vilivyojaribu kuingia katika ardhi ya Urusi vimerudishwa nyuma.