1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raisi ayalaumu mataifa ya Magharibi kuchochea ushoga

13 Julai 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amelaani kile alichokiita mitazamo ya nchi za Magharibi kuhusu ushoga na kusema mataifa hayo yanalikuza suala hilo ili kujaribu kumaliza "kizazi cha wanaadamu" kinyume na urithi wa tamaduni.

https://p.dw.com/p/4ToZr
Irans Präsident Raisi beginnt eine Afrikareise durch drei Länder in Uganda
Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Rais aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake mjini Kampala, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ambaye hivi karibuni alitia saini muswada wa sheria unaotoa adhabu kali ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifo kwa kosa linalotajwa kuwa "ushoga uliokithiri".

Awali, Ebrahim Rais alikuwa nchini Kenya ambako alifanya mazungumzo na Rais William Ruto.

Soma zaidi: Rais wa Iran Ibrahim Raisi aanzia Kenya katika ziara yake kwenye nchi tatu za barani Afrika

Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Iran barani Afrika kwa miaka 11 iliyopita.

Siku ya Alhamis (Julai 13), kiongozi huyo alitazamiwa kuelekea nchini Zimbabwe ambako alikuwa amepangiwa kuwa na mazungumzo na Rais Emmerson Mnangagwa. 

Ziara hiyo ya nadra ya kiongozi huyo wa Iran barani Afrika inafanyika wakati nchi hiyo ikikabiliwa na vikwazo vikali vya kiuchumi vya Marekani na hivyo inajaribu kuimarisha ushirikiano na madola mengine duniani.