1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF yasitisha mapigano kupisha Eid-ul-Adh'ha

Sylvia Mwehozi
27 Juni 2023

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa RSF wanaopambana na jeshi nchini Sudan, Mohamed Hamdan Daglo, ametangaza makubaliano ya upande mmoja ya kusitisha mapigano wakati wa sikukuu ya Eid-ul-Adh'ha.

https://p.dw.com/p/4T6RN
Sudan Khartum | Kämpfe zwischen Armee und RSF-Miliz | General Mohamed Hamdan Dagalo
Picha: MOHAMED NURELDIN ABDALLAH/REUTERS

Katika ripoti iliyorushwa na kituo cha televisheni cha Al-Arabiya siku ya Jumatatu (Juni 26), Daglo alisema usitishaji mapigano huo utakuwa kwa Jumanne na Jumatano.

Jeshi la Sudan pia lilithibitisha siku ya Jumatatu taarifa za wanamgambo wa RSF kudhibiti kambi kubwa ya kituo cha polisi iliyokuwa imesheheni silaha nzito.

Soma zaidi: Miezi miwili ya vita vya mateso kwa raia wa Sudan
Wanamgambo wa RSF walishutumu jeshi kushambulia hospitali

RSF walidai kwamba walikamata mamia ya magari ya mapigano na silaha baada ya kukidhibiti makao makuu ya polisi wa akiba mapema siku ya Jumapili.

Kumekuwa na ripoti za kuenea kwa mapigano kwa mara ya kwanza katika jimbo la Blue Nile karibu na mpaka na Ethiopia, ambako wakaazi walisema kundi la waasi lilishambulia maeneo ya jeshi.