SiasaSudan Kusini
Ulaya yakanusha madai ya kuvuruga uchaguzi wa Sudan Kusini
31 Mei 2024Matangazo
Naibu Mkuu wa Ujumbe huo, Lothar Jaschke amesema wao wanaunga mkono kikamilifu mazingira yatakayowezesha uchaguzi kufanyika kwa kuzingatia katiba na haki.
Kiir amedai kwamba mataifa yenye nguvu ya Magharibi yanataka kuuchelewesha uchaguzi nchini mwake lakini hakueleza zaidi kinachofanyika.
Kiongozi huyo wa Sudan Kusini amesema atahakikisha uchaguzi unafanyika Desemba kama ilivyopangwa na ametahadharisha kwamba iwapo utaahirishwa basi hatua hiyo itazua vurugu.
Ingawa Sudan Kusini inatazamiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza katika mwezi huo wa Desemba lakini michakato muhimu ambayo ni pamoja na katiba ya kudumu na jeshi la polisi moja kwa nchi hiyo bado havipo.