SAMSUN: Maandamano ya upinzani nchini Uturuki
20 Mei 2007Matangazo
Maelfu ya watu wamekusanyika katika mji wa bandari Samsun nchini Uturuki kuandamana dhidi ya serikali.Hayo ni sehemu ya maandamano yanayofanywa sehemu mbali mbali nchini humo.Waturuki wengi wanaamini kuwa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan na chama chake cha AK wanajaribu kuanzisha agenda ya Kiislamu nchini humo.Erdogan amelazimika kuitisha mapema uchaguzi mkuu kwa sababu ya shinikizo la umma na jeshi.Uchaguzi huo utakaotenzua mzozo unaohusika na suala la rais mpya,sasa unatazamiwa kufanywa mwezi wa Julai.