Scholz atangaza nchi yake itapeleka silaha zaidi Ukraine
16 Machi 2023Matangazo
Scholz ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi alipowasilisha taarifa ya serikali kuhusu mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika wiki ijayo.
Amesema pamoja na washirika wake wa Ulaya, Ujerumani itahakikisha kwamba Ukraine inapokea silaha na vifaa vya kujilinda. Ujerumani tayari inatoa msaada mkubwa wa silaha kwa Ukraine, kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya Urusi.
Viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya watajadili masuala ya ushindani wa kibiashara, nishati, na vita vya Ukraine, mjini Brussels wiki ijayo kwenye mkutano wao wa kilele.