Scholz kukutana na Merz katika midahalo kabla Februari 23
17 Desemba 2024Matangazo
Vituo vya televisheni vya Ujerumani, ARD na ZDF, vimepanga kufanya mdahalo wa kwanza Februari 9 huku kituo chengine cha binafsi, RTL, na jarida la Stern vikiwaalika wagombea hao katika mdahalo utakaofanyika Februari 16.Scholzanayetokea chama cha Social Democrat (SPD) alishindwa hapo jana katika kura ya imani aliyoiitisha bungeni kuona iwapo wabunge bado wana imani na serikali yake. Hatua hiyo imetoa muda wa siku 21 kwa Rais Frank Walter Steinmeier kulivunja bunge na kufanyika uchaguzi wa mapema.Muungano wa CDU-CSU wa Merz umeonekana kuwa juu ya chama cha SPD, hii ikiwa ni kulingana na kura ya maoni.