1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Ninao mkakati wa kuisaidia Ukraine na Trump

7 Desemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ana imani kwamba ataweza kukubaliana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump kwenye mkakati wa pamoja wa kuisaidia Ukraine baada ya kuzungumza naye kwa simu.

https://p.dw.com/p/4nrsd
Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Frederic Kern/Future Image/IMAGO

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ana imani kwamba ataweza kukubaliana na Rais mteule wa Marekani  Donald Trump kwenye mkakati wa pamoja wa kuisaidia Ukraine baada ya kuzungumza naye kwa simu. Scholz ameyasema katika mahojiano na gazeti la Funke.

Kansela huyo ameongeza kuwa anao ujasiri wa kuendeleza mkakati wake wa Ukraine wa kuipa msaada nchi hiyo na kwamba timu yake kwa sasa imefanya majadiliano na washauri nwa ulinzi wa Trump juu ya suala hilo.

Soma zaidi: Mashambulizi ya Urusi yauwa 12 Zaporizhzhya

Suala la Ukraine ni moja ya ajenda kubwa katika kampeni za uchaguzi wa Ujerumanin utakaofanyika mwezi Februari baada ya kusambaratika kwa serikali ya muungano wa vyama vitatu.Friedrich Merz, kiongozi wa upinzani wa kihafidhina wa Ujerumani ambaye yupo kwenye kinyang'anyiro cha kumg'oa ukansela Scholz amesema Ujerumani inapaswa kutuma makombora ya Taurus kwa ukraine hatua ambayo Scholz ameipinga akisema kuwa itazidisha vita.

Hivi karibuni Scholz alifanya ziara ya ghafla mjini Kyiv na kuahidi msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine.