Serikali ya Barnier wa Ufaransa yaangushwa bungeni
5 Desemba 2024Matangazo
Kura hiyo iliungwa mkono na wabunge wa mrengo wa shoto na mrengo mkali wa kulia, kwa wingi wa kura 331.
Vyama hivyo vilikerwa na hatua ya Barnier kutaka kutumia nguvu maalum za kikatiba kukwepa maamuzi ya bunge juu ya bajeti. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuondolewa madarakani kwa kura ya bunge tangu mwaka 1962.
Soma zaidi: Wabunge waiangusha serikali Ufaransa
Barnier, mwanasiasa mkongwe wa Kifaransa aliyejizolea umashuhuri kwa kuongoza mazungumzo ya Uingereza kujitowa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit, aliteuliwa na Rais Emmanuel Macron kuwa waziri mkuu mnamo mwezi Septemba mwaka huu.
Rais Macron anatazamiwa kuhutubia taifa jioni ya leo na vyanzo vinasema huenda akamtangaza waziri mkuu mpya kabla ya Jumamosi.