1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la itikadi kali Mali laua watu 77

19 Septemba 2024

Mamlaka za usalama za Mali zimesema hivi leo kuwa shambulio la siku ya Jumanne wiki hii lililofanywa na wapiganaji wenye itikadi kali katika mji mkuu Bamako, lilisababisha vifo vya watu 77 na wengine 255 walijeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4krHx
Mali Bamako | Moshi baada ya mashambulizi kwenye kambi ya kijeshi
Maafisa wa usalama wa Mali wakimshikilia mtu baada ya jeshi la Mali kusema kuwa kambi ya mafunzo ya kijeshi katika mji mkuu Bamako imeshambuliwa mapema Jumanne, Septemba 17, 2024. Picha: AP Photo/picture alliance

Hati ya siri iliyothibitishwa imesema idadi ya vifo imefikia karibu 100 ingawa serikali ya kijeshi ya Mali haijatoa idadi rasmi ya waliouawa kwenye mashambulizi hayo, yanayodaiwa kuendeshwa na kundi la itikadi kali la JNIM lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al-Qaeda. Shambulio hilo lilijiri siku moja baada ya mataifa matatu ya kanda ya Sahel yanayoongozwa kijeshi ya Mali, Niger na Burkina Faso kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuundwa kwa kundi lao lililojitenga.