1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoCameroon

Shirikisho la Soka Cameroon lapinga hatua ya Eto'o kujiuzulu

6 Februari 2024

Nyota wa zamani wa kandanda Samuel Eto'o ametangaza hapo jana kujiuzulu katika wadhifa wake wa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon.

https://p.dw.com/p/4c56H
Nyota wa soka wa zamani Samuel Eto'o
Nyota wa zamani wa kandanda Samuel Eto´o ambaye sasa ni Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon: 12.09.2019Picha: Rodrigo Jimenez/Agencia EFE/imago images

Uamuzi huo wa Eto'o umekataliwa na kamati yake ya kiutendaji ambayo imesema bado inamuamini.

Eto'o mwenye rekodi ya mchezaji bora wa Afrika mara nne  na ambaye ameshikilia wadhifa huo wa Rais wa shirikisho la Soka la Cameroon tangu Desemba 11 mwaka 2021, amekuwa akikabiliwa na tuhuma za mienendo isiyofaa, upangaji matokeo na rushwa.

Hatma ya Kocha wa Cameroon Rigobert Song iko pia matatani baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON inayoendelea huko Ivory Coast.