Simba kugharamia uharibifu wa baada ya mechi ya CAF
16 Desemba 2024Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya michezo, imeitaka Simba kugharamia uharibifu uliosababishwa na mashabiki waliong'oa na kuvunja viti. Vurugu zilifuatia bao la ushindi la Simba ambalo lilifungwa katika dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza.
Mashabiki wa timu zote waling'oa na kurushiana viti. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya michezo Gerson Msigwa imesema Simba SC itagharamia hasara yote iliyotokea. Ushindi wa 2 – 1 unaiweka Simba katika nafasi ya tatu ya Kundi A na pointi 6 sawa na Constantine iliyoko nafasi ya pili. F.C. Bravos do Maquis inakamata usukani na pointi 6.
Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, miamba Yanga inaburuza mkia katika Kundi A baada ya sare ya 1 – 1 na TP Mazembe. Ina pointi moja huku Al Hilal ikiongoza na pointi 9. MC Alger ni ya pili na pointi nne huku Mazembe ikiwa ya tatu na alama mbili.
Mjini Kigali, Timu ya taifa ya Rwanda "Amavubi” yaanza maandalizi dhidi ya Sudan Kusini kuelekea Fainali za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani (CHAN) wakati Rais wa Rwanda Paul Kagame akitangaza rasmi kuwa Kigali inapania kuwa mwenyeji wa mashindano ya mbio za magari ya Langalanga maarufu kama Formula One. Mengi zaidi na Mwanmichezo wetu Christopher Karenzi