Somalia: Wanajeshi walioko Eritrea kurejea nyumbani Disemba
20 Desemba 2022Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na raia wa Somalia wanaoishi Marekani wakati wa ziara yake nchini humo. Kwa miezi kadhaa, uvumi ulienea Somalia kwamba wanajeshi hao huenda wakapelekwa katika eneo linalokabiliwa na vita la Tigray, nchini Ethiopia.
Mohamud ambaye aliahidi kuwarejesha nyumbani wanajeshi wakati wa kampeni yake, aliwatembelea katika kambi za mafunzo nchini Eritrea, mwezi Julai.
soma zaidi:Hoteli iliyoshambuliwa na Al Shabaab yadhibitiwa Somalia
Mwezi Juni, mwaka uliopita, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadaamu nchini Eritrea, Mohamed Abdelsalam Babiker, alizungumzia taarifa kwamba wanajeshi wa Somalia waliondolewa katika kambi za mafunzo ya kijeshi nchini Eritrea na kupelekwa kwenye uwanja wa vita huko Tigray, ambako waliongozana na wanajeshi wa Eritrea ambao wanaviunga mkono vikosi vya shirikisho vya Ethiopia kupambana na waasi.