1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSri Lanka

Sri Lanka yafanya uchaguzi wa kwanza tangu maandamano

21 Septemba 2024

Raia wa Sri Lanka watamchagua rais mpya katika uchaguzi wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliyochochewa na mgogoro wa kiuchumi kufanyika na yaliomuondoa madarakani Rais Gotabaya Rajapaksa mnamo mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/4kvBW
BG Präsidentschaftskandidaten Sri Lanka
Rais wa Sri Lanka Ranil WickremesinghePicha: REUTERS/Dinuka Liyanawatte

Zaidi ya watu milioni 17 kati ya milioni 22 nchini humo wamejiandikisha kama wapiga kura katika uchaguzi wa urais ambao unaonekana kuwa mbio kati ya Rais aliyeko madarakani Ranil Wickremesinghe, kiongozi mkuu wa upinzani Sajith Premadasa na Anura Kumara Dissanayake anayeegemea siasa za mrengo wa kushoto.

Zoezi la kupiga kura linatarajiwa kuanza kuanzia saa moja asubuhi na kukamilika saa kumi alasiri huku kura zikianza kuhesabiwa muda mfupi tu baada ya hapo.

Soma pia:  Sri Lanka hatimae yapewa fedha na IMF za kuinusuru kiuchumi

Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu nchi hiyo itumbukie kwenye mgogoro wa kiuchumi mwaka 2022 na kuifanya kushindwa kulipigia fedha za uagizaji wa bidhaa muhimu ikiwemo mafuta, dawa na gesi ya kupikia.

Maelfu ya watu waliandamana mjini Colombo na kuivamia ofisi na makaazi rasmi ya rais, na kumlazimisha rais Gotabaya Rajapaksa kuikimbia nchi na baadaye kujiuzulu.