1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan kukabiliwa na viwango vikubwa vya njaa

24 Desemba 2024

Mamlaka ya kimataifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa IPC kuhusu upatikanaji wa chakula imesema njaa imesambaa kote katika taifa linalokumbwa na vita la Sudan.

https://p.dw.com/p/4oYRf
Sudan
Sudan ipo katika hatari ya kukabiliwa na viwango vikubwa vya njaa Picha: Maura Ajak/AP/picture alliance

IPC imesema njaa inatarajiwa kuzidi kuenea huku makambi ya wakimbizi na jamii zilizopoteza makazi zikiathirika pakubwa. 

Mamlaka hiyo ya kimataifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, imesema njaa hiyo tayari imeshaathiri makambi mawili ya wakimbizi upande wa Magharibi  na Kusini na watu zaidi ya 638,000 wanakabiliwa na viwango vya kutisha vya njaa huku wengine milioni 8.1 wakiwa katika hatari ya njaa.

Kilicho nyuma ya vita ambacho kinasababisha njaa Sudan

IPC imesema kati ya mwezi Desemba na mwezi May watu milioni 24.6 ambayo ni nusu ya idadi jumla ya watu wa Sudan wanakadiriwa kukabiliwa na viwango hivyo vikubwa vya upungufu wa chakula. 

Sudan imekuwa katika vira vya wenyewe kwa wenyewe kwa miezi 20 sasa  baada ya mzozo mkali kati ya makundi mawili ya kijeshi.