Kulingana na mashirika ya umoja wa mataifa, mkoa wa Shinyanga uliopo kaskazini mwa Tanzania unaongoza kwa kua na tatizo la mimba na ndoa za utotoni nchini humo na zaidi ya wanafunzi 500 hupatiwa ujauzito kila mwaka. Jamii inasema kwamba miongoni mwa sababu zinazochangia hali hiyo ni imani za kishirikina ambapo wanaume huambiwa wakutane kimwili na mabinti wadogo ili waweze kupata utajiri.